Mugabe atazamia kuwa Mkulima, asema jamaa yake

Mpwa wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema Mugabe yuko buheri wa afya na mwenye tabasamu baada ya kushurutishwa kujiuzulu baada ya kutawala nchi hiyo katika muda wa miaka 37. Leo Mugabe, mwanawe dadaye Mugabe marehemu A�Sabina amesema Mugabe anatazamia kuanza ukulima na kukaa nyumbani kwake katika sehemu za mashambani. Ameongeza kuwa mkeweA�Mugabe Grace sasa anaangazia zaidi mipango ya kujenga chuo kikuu kwa heshima yake. Hata hivyo Leo amekataa kuelezea kuhusu malimbikizi ya dola milioni kumi zinazosemekana zimetolewa kwa Mugabe kama sehemu ya makubaliano ya kujiuzulu kwake.