Mugabe akataa wito wa kumtaka kujiuzulu

Mashauriano yanayoongozwa  na jeshi  yanatarajiwa  kuendelea  baada ya Rais  Robert Mugabe wa Zimbabwe kukataa kujiuzulu  kufuatia mkutano na wakuu  jeshi ambao wamenyakua uongozi  wa  taifa hilo. Leo ni siku ya tatu tangu wakuu wa jeshi wadhibiti uongozi  nchini Zimbabwe  wakisema wanataka kuwakabili wahalifu wanaomzunguka Rais   Robert Mugabe ingawa hawakutaja majina.  Jeshi lilimzuilia   Mugabe nyumbani kwake huku wakiwatia mbaroni  mawaziri wake kadhaa ambao wanaohusika na mzozo wa kirika  uanokumba chama tawala nchini humo cha  Zanu-PF. Mhudumu wa aliyekuwa makamu wa Rais wa  Zimbabwe  Emmerson Mnangagwa, ambaye kutimuliwa kwake kazini  juma lililopita  kulichangia jeshi kutwaa uongozi  amesema leo kuwa kiongozi huyo  amerejea nchini humo. Mashauriano katika mji mkuu wa  Zimbabwe, yaliandaliwa baada ya siku chache zizilokumbwa na hali  ya wasiwasi baada ya wanajeshi kufunfgabarabara zote, kudhibiti kituo cha televisheni cha kitaifa  na kumzuilia kiongozi  huyo mnkongwe nyumnbani kwake.