Mudavadi Awahimiza Wakaazi Wa Busia Kujisajilisha Kupiga Kura

Kiongozi wa chama cha Alliance National Congress, Musalia Mudavadi, amewahimiza wakazi wa magharibi ya nchi kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa kuwa wapiga kura.Mudavadi alisema ipo haja ya kutumia mbinu zote ili kuhakikisha Wakenya wamesajiliwa kuwa wapiga kura.Akiongea wakati wa harambee katika kanisa la Kianglikana la Nambale katika kaunti ya Busia, Mudavadi alisema ni kupitia kwa kupiga kura ndipo Wakenya watapata fursa ya kujichagulia kiongozi wampendaye.Vingozi wengine waliohudhuruia sherehe hiyo ni pamoja na gavana wa kaunti ya Busia, Sospeter Ojaamong, mbunge wa Nambale, John Bunyasi, mbunge wa Sabatia Alfred Agoyi, na mbunge wa Lugari Ayub Savula. Viongozi hao walisisitiza haja ya umoja miongoni mwa viongozi kutoka eneo la magharibi ya nchini ili kuwawezesha kuteua muwaniaji mmoja wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.