Muda wa kutafuta vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi imeongezwa kwa muda wa wiki nne

Wizara ya usalama wa kitaifa na ushirikishi wa taifa imeongeza muda wa kutafuta vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi kwa minajili ya kusajiliwa kwa wiki nne. Hata hivyo baadhi ya wakenya wangali wanasubiri dakika za mwisho ili kuanza pilkapilka za kupanga foleni ndefu katika vituo vya kusajiliwa. Katika kaunti yaA�A�Narok foleni katika afisi za usajili wa watu zilipungua ikilinganishwa na siku kumi zilizopita ambapo wakazi walimiminika katika afisi hizo wakijaribu kupata vyeti hivyo kabla ya kukamilika kwa makataa iliyokuwa imewekwa. Afisa wa usajili wa watu katika kaunti ya NarokA�A�Douglas Masinde alipongeza juhudi za serikali za kuongeza muda huo wa makataa hukua akiongeza kuwa utasaidia kupunguza mrundiko wa kazi katika afisi hizo. Masinde alisema kuwa kufikia sasa vyeti elfuA�A�30 vya kuzaliwa vimetolewa huku vingine elfu 20 vikisubiri kutolewa. Alitoa wito kwa wazazi kutumia vyema muda ulioongezwa na kukoma pilkapilka za dakika za mwisho. Aliongeza kuwa kuna vyeti vingi ambavyo vimetayarishwa na lakini wenyewe hawajakuja kuvichukuwa. Alitoa wito kwa wakazi kujitokeza kwa idadi kubwa na kuhakikisha kuwa wanasajaliwa kwa wakati ufaao ili kurahisisha utayarishaji wa mipango.