Mtu mmoja zaidi afariki katika mafarakano ya kisiasa Venezuela

Idadi ya watu waliofariki kutokana na maandamano nchini VenezuelaA� imeongezeka .Hii ni baada ya mwanamke mmoja aliyejeruhiwa kwenye maandamano ya kuunga mkono serikali kufariki .Zaidi ya watu 10 wameuawa mwezi huu kwenye maandamano kati ya watetezi na wapinzani wa serikaliA� nchini humo,hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo Caracas.Taharuki imetanda nchini humo tangu mwisho wa mwezi uliopita,kufwatia uamuzi wa mahakama ya juu nchini humo kuchukua mamlaka ya bunge la taifa, ambalo wanachama wake wengi ni wafwasi wa upinzani. Wakosoaji wa serikali walitaja uamuzi huo kuwa ukiukaji wa katiba ,hasa kifungu kinachohusu ugawanaji mamlaka kati ya asasi za serikali.Uamuzi huo wa mahakama hata hivyo ulibatilishwa siku tatu baadaye,lakini hadi sasa haujafanikiwa kutuliza ghasia nchini humo.