Mtoto wa mwezi mmoja anusurika kifo

Mvulana mmoja kutoka Uchina aliyedhaniwa kuwa kafariki alinusururika kuchomwa kwenye tanuri pale alipoanza kulia. Wazazi wa mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja walikuwa wamekubali kusitisha matibabu yake kwenye hospitali ya mkoa huko Anhui mashariki mwa Uchina. Wahudumu walidhibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa amefariki na mwili wake ukapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti. Hata hivyo mtoto huyo alianza kulia akiwa chumbani humo na akarejeshwa mara moja hospitalini. Daktari mmoja amesimamishwa kazi na muuguzi kuachishwa kazi kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukianzishwa. A�

A�