Mtihani wa K C P E kuanza tarehe 31 Octoba

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane-KCPE, utaanza tarehe 31 mwezi Oktoba. Waziri wa elimu, dakta Fred Matianga��i alisema mtihani huo utafanywa kwa kipindi cha siku-3. Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne-KCSE wa maandishi utaanza tarehe 6 mwezi Novemba, huku ule wa mazungumzo ukianza tarehe 23 mwezi Oktoba. Dakta Matianga��i sasa anaihimiza tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC izingatie kalenda ya mtihani wakati wa kutenga tarehe yake ya marudio ya uchaguzi wa urais. Aliihimiza tume ya IEBC iandae uchaguzi huo kabla ya tarehe 17 mwezi Oktoba ikitilia maanani hatma ya watahiniwa ambao wataathiriwa kalenda hiyo ikivurugwa. Aidha alithibitisha kwamba shughuli za masomo hazitatatizwa katika shule zitakazotumiwa kama vituo vya kupiga kura ikiwa tume hiyo ya uchaguzi itazingatia pendekezo hilo la wizara ya elimu.A�