Mtalii Wa Marekani Auwawa Na Wengine Kumi Kujeruhiwa Katika Shambulio La Jaffa

Mtalii mmoja wa Marekani ameuliwa na watu kadhaa  kujeruhiwa kwenye mashambulizi dhidi ya raia wa Israel karibu na miji ya Tel Aviv na Jerusalem.Kwa mujibu wa polisi wa Israel,mtalii huyo kwa jina Taylor Force alikuwa miongoni mwa watu 10 waliodungwa visu na mshambulizi mmoja katika mji wa Jaffa,kusini mwa mji wa Tel Aviv.Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden alikuwa akihudhuria hafla moja umbali mdogo kutoka mahala hapo.Awali,maafisa wawili wa polisi waliuliwa  kwa kupigwa risasi, mashariki ya mji  wa Jerusalem.Polisi walisema kuwa washambulizi hao ambao walikuwa  wapalastina waliuliwa wote.