Mtaalam wa maswala ya kiuchumi atarajiwa kuhojiwa leo

Mtaalam wa maswala ya kiuchumi David Ndii anatarajiwa kuhojiwa leo A�katika makao makuu ya idara ya uplelezi kwenye barabara ya Kiambu. A�Ndii ataandikisha taarifa na maafisa wa kitengo cha uhalifu sugu kutokana na madai ya uchochezi. A�Duru zinaashiria kuwa uvamizi kwenye hoteli moja katika kaunti ya Kwale ulitekelezwa na maafisa sita wa polisi mbele ya mlinzi mkuu wa hoteli hiyo. Alizuiliwa kwa muda katika kituo kimoja cha polisi huko A�Ukunda kabla ya kuhamishwa hadi katika idara ya upelelezi jijini Nairobi kwa mahojiano. Yeye huandika jarida katika gazeti la Daily Nation ambapo huchapisha maoni ya watu yanayomkosoa pakubwa rais Uhuru Kenyatta na serikali yake hasa yakihoji ajenda yake ya kiuchumi , utekelezaji na matumizi . AidhaA� Ndii ni mmoja wa waratibu wa mikakati wa muungano wa NASA. Wakati huo huo wanasiasa wa mrengo wa NASA na mawakili wakiongozwa na seneta wa Siaya James Orengo wamekita kambi katika makao makuu ya idara ya upelelezi jijini Nairobi ambapo imesemekana A�Ndii anazuiliwa. Viongozi hao wanataka kuruhusiwa kumwona Ndii na pia kuzungumza na maafisa wanaofanya upelelezi.