Msukosuko wa kisiasa umedunisha biashara ya utalii

Kipindi kirefu cha kampeini A�za uchaguzi hapa nchini kimeathiri biashara. Chama cha maajenti wa safari za kitalii-KATA kimesema kuwa ingawa sekta ya utalii imestahimili changamoto zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe-8 Agosti, msukosuko wa kisiasa hapa nchini pamoja na maandamano vimedunisha biashara ya utalii. Kwenye taarifa, afisa mkuu mtendaji wa chama cha KATA, Nicanor Sabula amesema biashara ya kusafirisha watalii hutoa nafasi za ajira kwa maelfu ya wakenya kote nchini. Sabula A�amesema hali ya sasa ya kisiasa imesambaratisha biashara. Aliongeza kuwa kufutiliwa mbali kwa makongamano kadhaa hapa nchini miongoni mwayo kongamano la shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana ukimwi-UNAIDS ni ishara tosha ya matatizo yanayokumba sekta ya utalii. Idadi ya watalii wanaonuia kuzuru hapa nchini imepungua kwa asilimia-10 katika kipindi kilichomalizika mwezi Septemba ikilinganishwa na kipindi sawia mwaka uliopita. Aidha, Sabula A�alisema hatua ya serikali ya kukatiza safari za maafisa wake katika nchi za nje imepunguza mapato ya sekta ya utalii kwani serikali huchangia zaidi ya asilimia-60 ya safari za kitalii.