Msichana Mwenye Kiota Cha Siafu Kichwani

Msichana wa umri wa miaka-12 aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya masikio amewashangaza madaktari ilipogunduliwa kwamba alikuwa na kiota cha siafu kichwani kwake. Kufikia sasa madaktari wametoa siafu elfu moja kwenye masikio ya msichana huyo kwa jina Shreya Darji huku wakiendelea kustaajabu jinsi wadudu hao walivyoingia kichwani mwa msichana huyo na hata kuzaana. Yamkini siafu kumi hudondoka kutoka kichwa cha msichana huyo kila siku kupitia masikio yake. Mtaalamu wa magonjwa ya masikio, pua na kifua Dr Jawahar Talsania anasema wamejaribu kila mbinu kuwaondoa wadudu hao kichwani mwa msichana huyo lakini wadudu hao wanaendelea kuzaana. Babaye msichana huyo, Sanjay Darji amesema sasa wanaomba muujiza utendeke kwani wamejaribu kila aina ya matibabu wakiwemo waganga lakini hawajafaulu.