Mshukiwa wa ugaidi akamatwa

Mtaalam wa vilipuzi katika kundi laA�Al-Shabaab ni miongoni mwa washukiwa kadhaa wa ugaidi waliokamatwa kuhusiana na mashambulizi yaliyotokea katika kaunti ya Mandera. Kwenye taarifa Inspekta Jenerali wa polisi Joseph Boinnet amesema mtuhumiwa huyo,A�Ahmed Abdi Yare anasaidia polisi katika uchunguzi wao. Mtuhumiwa huyo alinaswa na silaha na vifaa vya kutengenezea vilipuzi. Aidha, polisi wameimarisha msako dhidi ya ugaidi katika eneo hilo kwa lengo la kuwatokomeza magaidi ambao wameingia katika eneo hilo kutoka Somalia. Boinnet pia amesema wanafuatilia habari kuwa mashambulizi hayo yanahusiana na ulanguzi wa mihadarati na vitendo vingine vyaA�uhalifu. A�Wakati huo huo, Boinnet ametahadharisha kuwa kundi la A�al shabab huenda linapanga kutekeleza mashambulizi zaidi hapa nchini huku Waislamu wakitarajia kuanza mfungo wa Ramadhan. Alisema magaidi hao huenda wakatatiza sherehe hizo kwa kutekeleza mashambulizi zaidi.A�Boinnett amewataka wakenya kuripoti vitendo vyovyote wanavyoshuku kupitia nambari ya simu-999, 911 au atafaA�112 ambazo hazina malipo. Huduma ya taifa ya polisi imepata pigo katika muda wa siku mbili zilizopita kutokana na mauaji ya maafisa wake-13.