Msanii Wa Nyimbo Za Injili Ashtakiwa Kwa Wizi Wa Mamilioni

Msanii mmoja wa Kike wa nyimbo za Injili pamoja na watu wengine wane walioshtakiwa kwa kuiba zaidi ya shilingi milioni- 27 kutoka kwa serikali ya Kaunti ya Kitui atafikishwa kuzimbani kwa mara ya tatu mnamo tarehe 18 mwezi Marchi mwaka huu wa, 2016 wakati kesi yao itakapounganishwa na na ile ya washukiwa wengine wawili ambao walifikishwa mahakamani hapo jana. Washukiwa hao Erastus Ngura na Elizabeth Mwende walikanusha mashtaka dhidi yao jana mbele ya hakimu mwandamizi wa Kitui Maryanne Murage na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu-100 kila mmoja pesa taslimu. Ngura na Mwende walikamatwa juzi Jumanne na kufikishwa mahakamani kufuatia uchunguzi zaidi kuhusiana na kesi hiyo. Msanii huyo Faith Kithele na Alex Kioko walishtakiwa mara ya kwanza tarehe 18 Januari baada ya kesi yao kuunganishwa na ile ya Sarah Wangui, Mary Waithera na Margaret Musee ambao walikuwa wameshtakiwa tarehe 4 Januari.