Serikali yaanzisha mikakati ya kufadhili upanuzi wa reli ya Naivasha- Narok

Serikali imeanzisha mashauriano ya kufadhili mradi wa upanuzi wa reli ya kisasa kutoka Naivasha hadi Narok, Bomet, Nyamira na Kisumu. Waziri wa uchukuzi James Macharia amesema kandarasi ya upanuzi wa reli hiyo katika sehemu hizo tayari imetiwa saini, na kwamba mradi huo utagharimu shilingi bilioni-350. Alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa bandari ya bara huko Kisumu itakayoshughulikia mizigo inayosafirishwa kutoka ziwa A�Victoria hadi mataifa jirani kwa thamani ya shilingi bilioni-14. Tanzania imeanzisha ujenzi wa reli yake ya umbali wa kilomita 422 itakayogharimu shilingi milioni 192 za Kenya, hatua ambayo Macharia alisema haitathiri harakati za ushirikiano wa kikanda. A�

A�