Mpwa wa Mnangagwa atoa wito wa kusamehewa kwa washirika wa karibu wa Grace Mugabe

Mpwa wa rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameripotiwa kutoa wito kwa kusamehewa kwa washirika wa karibu wa Grace Mugabe mkewe aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo,akisema wakati umewadia kwa chama tawala nchini humo cha Zanu-PF A�kudumisha umoja wake.Akiongea wakati wa hafla ya kusherekea kuapishwa kwa rais A�Mnangagwa huko Dema, Tongai Mnangagwa alisema wandani wa Grace Mugabe katika chama tawala walipotoshwa.Aliongeza kuwa wakati umewadia kwa umoja wa chama kudumishwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.