Mourinho Ataka Kuakikishiwa Ukufunzi wa Manchester United

Aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho anataka kuhakikishiwa, kwa stakabadhi, kuwa atachukua wadhifa wa mkufunzi wa Manchester United Louis van Gaal mwishoni mwa msimu huu.

Ripoti nchini Uingereza zimetangaza kuwa licha ya Mourinho kuhakikishiwa kuwa atachukua wadhifa wa ukufunzi katika kilabu hicho, aliyekuwa kocha Alex Ferguson angali anamuunga mkono Louis Van Gaal.

Chelsea ilimpiga kalamu kocha Mourinho mwaka jana, miezi saba baada ya kuiongoza Chelsea kutwaa taji ya ligi kuu nchini Uingereza.