Mourinho Adai Manu Itamaliza Kwa Nne Bora

Jose Mourinho amesisitiza kuwa Manchester United huenda ikamaliza katika nafasi nne bora katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

United kwa sasa inashikilia nafasi ya sita baada ya kushinda mechi tatu mfululizo, alama nne nyuma ya timu inayoorodheshwa katika nafasi ya nne. Timu hiyo haikufuzu ligi ya mabingwa Barani Ulaya msimu uliopita chini ya ukufunzi wa Louis Van Gaal, na Mourinho amedhihirisha nia yake ya kuiongoza timu hiyo kumaliza katika nafasi bora licha ya ushindani mkali.