Moto ulioteketeza wanafunzi ulianzishwa kimaksudi

Moto uliozuka katika shule ya upili ya wasichana ya Moi jijini Nairobi jumamosi asubuhi ulianzishwa kimaksudi na haikuwa ajali. Akihutubia wanahabari hivi leo, waziri wa elimu Dr Fred Matiangi amesema kufikia sasa idadi ya wanafunzi waliofariki kwenye mkasa ahuo imefikia wanafunzi-9 baada ya mwanafunzi mwengine kufariki kutokana na majerahaA� ya moto. Hospitali ya Nairobi Women imethibitisha kwamba wanafunzi wawili kati ya kumi waliolazwa katika hospitili hiyo kufuatia mkasa huo, wangali katika hali mahututi. Kwa sasa uchunguzi wa DNA unafanywa kuwezesha wazazi kutambua watoto wao na kuandaa mazishi. Shule hiyo imefungwa kwa muda wa majuma mawili huku uchunguzi kuhusu mkasa huo ukiendelea.