Moses Wetanga��ula Atupilia Mbali Mwaliko Wa Eugene Wamalwa Kujiunga Na Muungano Wa Jubilee

Kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetanga��ula amekataa mwaliko wa waziri wa maji Eugene Wamalwa kujiunga na muungano wa Jubilee. Akiongea jana mjini Kitale, Wetanga��ula alisema hana nia ya kuondoka kwenye muungano wa CORD lakini badala yake atawania uteuzi wa uwaniaji urais kwa tiketi ya muungano wa Cord kwenye uchaguzi mkuu ujao. Seneta huyo wa Bungoma pia alitoa wito kwa wafuasi wa CORD wasichukulie maoni tofauti baina ya vinara wenza wa muungano huo kuwa ishara ya mizozo bali dhihirisho la demokrasia. Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa alisema ni kinaya na jambo la kushangaza kwamba chama cha New Ford Kenya kilichojiunga na muungano wa Jubilee kinawaalika viongozi wengine wa jamii ya Waluhya ilhali wao pia wamejiunga na muungano huo hivi maajuzi. Mnamo siku ya Jumamosi waziri wa maji Eugene Wamalwa alisema Wetanga��ula hana jingine ila kuugura muungano wa CORD kwani akijiunga na Jubilee itamaanisha kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kumshinda rais Uhuru Kenyatta.