Moses Kuria na Johnston Muthama wakamatwa kwa tuhuma za kueneza chuki

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnston Muthama walilala kwenye korokoro cha kituo cha polisi cha Pangani baada ya kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kueneza taarifa za chuki. Kuria alihojiwa jana alasiri katika makao makuu ya ujasusi yaliyoko kwenye barabara ya Kiambu, Jijini Nairobi, ambako alikuwa amezuiliwa kwa masaa kadhaa. Inadaiwa kwamba Kuria alichapisha makala kwenye ukurasa wa Facebook ambapo alimtusi kiongozi wa upinzani Raila Odinga na familia yake, akisema kwamba amekuwa kero kubwa kwa utawala wa Jubilee. Pia ilidaiwa alisema kwamba watu wote wasio wazaliwa wa kaunti ya Kiambu watafurushwa kutoka kaunti hiyo na kuchukuliwa hatua ambazo hakuzitaja. Kuria ameweza kutembelewa na mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Muranga��a Sabina Chege miongoni mwa wengine.A� Muthama alikamatwa na polisi katika eneo la Kangundo kuhusiana na taarifa za chuki alizodaiwa kutoa wakati wa mkutano wa NASA mwishoni mwa juma. Yeye pia aliaandikisha taarifa katika makao makuu ya gurugenzi ya uchunguzi wa jinaiA� (DCI) jijini Nairobi. Wawili hao wamezuiliwa katika kituo cha polisi cha Pangani. Kiongozi wa NASAA� – Raila Odinga na pia wabunge kadhaa akiwemo Seneta wa Siaya James Orengo, walimtembelea Muthama katika kituo hicho cha Polisi. Akihutubia wanahabari kwenye kituo cha polisi chaA� Pangani, Odinga alidai kwamba kukamatwa kwa Muthama ni sehemu ya njama za Jubilee za kuhujumu kampeini zake.