Moses Kuria na Johnstone Muthama waachiliwa kwa dhamana

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama, wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu-300, pia mthamini A�wa shilingi milioni-1 kila mmoja na wawili hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kueneza taarifa za chuki, waliagizwa na hakimu mkuu Francis Andayi kudumisha nidhamu njema A�hadi kusikizwa kwa A�kesi dhidi yao. Walitiwa nguvuni siku ya jumatatu kwa madai ya kueneza taarifa za chuki na kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Pangani. Kukamatwa kwao kuliibua hisia tofauti kutoka kwa wafuasi wa mirengo ya NASA na pia Jibilee, licha ya mbunge huyo wa Gatundu Kusini kuto-onyesha ishara zozote za kujuta kutokana na matamshi yake. Kuria alidaiwa kutoa matamshi yanayolenga watu wa jamii fulani ambao anadai walimpigia kura mgombeaji wa muungano wa NASA wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe 8 Augosti. Muthama kwa upande mwingine anatuhumiwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi wakati wa mkutano wa kampeini wa muungano wa NASA. Wote wawili walikuwa miongoni mwa wabunge waliokamatwa mwaka uliopita na kuzuiliwa kwenye kituo hicho-hicho cha polisi, kwa madai ya kueneza taarifa za chuki.