Monica Juma asema Kenya yapania kuwa mwanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa

Waziri wa mashauri ya kigeni Monica Juma amesema Kenya inapania A�kuwa mwanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kipindi cha kati ya mwaka 2021 na 2022.Akiongea leo katika hoteli moja hapa Nairobi,waziri huyo alisema serikali itaharakisha majadiliano ya mikataba ya kuwalinda wakenya wanaoishi ugaibuni.Akikiri kuwa ulanguzi wa binadamu ni biashara kubwa kwa makundi ya wahalifu,waziri huyo alihimiza ubadilishanaji wa A�habari za kijasusi katika eneo la abrika mashariki. Juma alisema afisi yake iko wazi kwa majadiliano na umma huku akitoa wito wa ushirikiano.