Monaca yakataa ombi la Man City kumsajili Benjamin Mendy

Monaco imetupilia mbali ombi la pauni milioni 44.5 la Manchester City la kumsajili A�mlinzi Benjamin Mendy. City inalenga kumleta Mendy uwanjani Etihad, baada ya kuandikisha rekodi ya kumsajili mlinzi kufuatia uhamisho wa Kyle Walker kutoka Tottenham Hotspurs kwa kima cha pauni milioni 50. Aidha, Monaco imekataa ombi la City la kumsajili Mendy, huku ikitaka kima hicho ili kumwachilia mchezaji huyo. A�Mendy alishinda taji ya ligi kuu nchini Ufaransa katika msimu wake wa kwanza na Monaco na pia akaisaidia timu hiyo, inayofunzwa na Leonardo Jardim, kufuzu kwa nusu fainali za ligi ya mabingwa Barani Ulaya. City inaangazia kumsajili mlinzi kufuatia kuondoka kwa Gael Clichy, licha ya mchezaji Danilo, ambaye anatarajiwa kujiunga na City kwa kima cha pauni milioni 26.5, kuchezea Real Madrid katika nafasi hiyo.