Moitel Ole Kenta Asema Pendekezo La Kuuganisha Vyama Tanzu Vya Muungano Wa Jubilee Lapaswa Kujadiliwa

Mbunge wa Narok Kaskazini, Moitalel ole Kenta amesema pendekezo la kuuganisha vyama tanzu vya muungano wa Jubilee linapaswa kujadiliwa na sio kulazimishiwa viongozi. Kenta ambaye alikuwa katika shule ya msingi ya Olenkasurai, eneo bunge la Narok Kaskazini, alikariri kwamba jamii ya Wa-Maasai imetengwa katika maendeleo na kwamba itafanya uamuzi wa busara wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.A�Mbunge huyo alisema licha ya eneo hilo kuchukuliwa kuwa ngome ya chama cha URP, jamii hiyo haitakubali kushurutishwa kuunga mkonoA�A�mrengo wowote wa kisiasa. Ole Kenta alitishia kuwahamasisha wakazi wajiunge na vyama vingine iwapo maswala yaliyowasilishwa kuhusu kuunganishwa kwa vyama tanzu vya muungano wa Jubilee, hayatatatuliwa. Alisema kesi aliyowasilisha mahakamani kuzuia shughuli hiyo, haijaamuliwa.