Mogadishu Kuaandaa Mkutano Wa 53 Wa Shirika La IGAD

FLAGS

Mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu, ambao miaka michache iliyopita uliorodheshwa kuwa mji hatari zaidi duniani, unajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 53 wa shirika la IGAD utakaoandaliwa mwishoni mwa juma kwa mara ya kwanza nchini humo.

Viongozi kutoka Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo litakaloangazia hali ya siasa na usalama nchini humo pamoja na uchaguzi ujao wa nchi hiyo ikiwemo hali ya kisiasa nchini Sudan kusini.

Kuna walinda amani elfu-22 wa jumuiya ya Afrika nchini Somalia, ambao wanasaidia jeshi la nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa al-Shabab, na kudumisha usalama katika taifa hilo. Nchi nne wanachama wa jumuiya hiyo zimepeleka wanajeshi wao kujiunga na kikosi hicho almaarufu AMISOM