Mo Farah anyakua makala ya kwanza ya mbio za nusu marathoni ,London

Mwingereza Mo Farah alimshinda Mkenya Daniel Wanjiru na kushinda makala ya kwanza ya mbio za nusu marathoni za London hapo jana, huku Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya tatu.

Bingwa huyo mara nne wa Olimpiki alishiriki kwenye mbio hizo za nusu marathoni kujiandaa kwa mbio za marathoni za London zitakazoandaliwa mwezi Aprili. Farah mwenye umri wa miaka 34 ananuia kuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza kushinda mbio za wanaume tangu mwaka 1993. Charlotte Purdue wa Uingereza alishinda mbio za akinadada mbele ya Lily Partridge na Charlotte Archer waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia