Mnangagwa kuapishwa Ijumaa kuwa rais wa Zibambwe

Kiongozi ambaye anapigiwa upato kuchukua wadhifa wa urais nchini Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesifia sura mpya ya demokrasia inayojitokeza nchini humo mara tu baada ya kurejea kutoka uhamishoni.Mnangagwa ameahidi kutoa nafasi za kazi kwa raia,huku ikikadiriwa kuwa takriban aslimia 90 ya watu nchini humo hawana kazi.Kulingana na runinga ya taifa hilo,Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa Zimbabwe siku ya ijumaa.Alikuwa uhamishoni nchini Afrika kusini,alikotorokea majuma mwili yaliopita baada ya kutimuliwa mamlakani kama makamu wa rais.Hatua hiyo ililazimisha majeshi ya nchi hiyo kuingilia kati na kumlazimuA� rais Mugabe ,ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 37 kunga��atuka uongozini.Mnangagwa aliwaambia wafwasi wake katika makao makuu ya chama cha ZANU-PF kuwa amenusurikaA� mara nyingi kuawa na kulishukuru jeshi la nchi hiyo kwa hatua ya kumwondoa Mugabe uongozini kwa amani.Hatibu wa chama cha ZANU-PF,alisema kuwa Mnangagwa mwenye umri wa miaka 71 atahudumu kwa kipindi cha utawala cha Mugabe kilichosalia hadi uchaguzi mkuu utakapofanywa nchini humo mwezi septemba mwaka ujao.