Mlinzi wa Wetangula afunguliwa mashtaka

Mlinzi wa seneta wa Bungoma Moses Wetanga��ula amefunguliwa mashtaka ya kuzua vurumai katika mahakama ya juu siku ya jumatatu. Simon Lonyia alishtakiwa kwa kuzua fujo na kumzuia afisa wa polisi kutekeleza wajibu wake na kuingia kwa lazima katika mahakama ya juu akiwa na bastola. Anadaiwa kumsukuma afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Central Robinson Thuku nje ya mahakama hiyo. Anadaiwa kutekeleza makosa hayo tarehe 28 mwezi huu. Alifikishwa mbele ya hakimu mkuu, Francis Andayi aliyemuachilia kwa dhamana ya shilingi 20,000 baada ya kukanusha shtaka hilo. Lonyia anawakilishwa na wakili Eunice Lumallas. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 18 mwezi ujao.