Mlinda lango wa Bayern Munich Manuel Neuer kukaa nje hadi mwisho wa msimu huu

Mlindalango wa Bayern Munich Manuel Neuer atakuwa nje hadi mwishoni mwa msimu huu baada ya kujeruhiwa kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Real Madrid jumanne iliyopita katika uwanjaA� wa Bernabeu.Neuer,A� alijeruhiwa wakatiA� Cristiano Ronaldo alipofunga bao la tatu katika muda wa ziada huku BayernA� ikibanduliwa kwa jumla ya mabao sita kwa matatu.A� Bayern Munich chini ya kocha Carlo Ancelotti inakaribia kunyakua taji yake ya tanoA� mfululizo yaA� Bundesliga.A� Aliyekuwa mlindalango waA� StuttgartA� Sven Ulreich, atachukua nafasi ya Neuer hadi mwishoni mwa msimu huu.A� Bayern Munich kesho itachuana naA� MainzA� inayokabiliwa na tishio la kuteremshwa ngazi.