Mkuu Wa Tume Ya Uchaguzi Gambia Aenda Mafichoni

Mkuu wa tume huru ya uchaguzi nchini Gambia amekwenda mafichoni na jamaa yake akihofia maisha yake, kulingana na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC. Kwa mujibu wa ripoti ambazo hazikuthibitishwa, Alieu Momar Njai, ambaye alitangaza kushindwa kwa rais Yahya Jammeh kwenye uchaguzi wa urais wa mwezi jana, ametoroka kutoka nchini humo. Awali rais Jammeh alikubali kushindwa kwenye uchaguzi huo, lakini akabadili msimamoA� baada ya muda mfupi na sasa amekataa kunga��atuka mamlakani.

Kiongozi huyo wa Gambia sasa ameamuru vikosi vya usalama kuzingira afisi za tume ya uchaguzi. Hata hivyo mwana wa kiume wa Njai hakuweza kuthibitisha ikiwa baba yake ametoroka, lakini alimtakia heri popote alipo. Rais Jammeh, ambaye ameitawala Gambia kwa miaka 22, anatarajiwa kukabidhi mamlaka kwa Adama Barrow, ambaye ni mmliliki na mjenzi waA� majumba, ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa urais uliofanywaA� tarehe mosi mwezi wa Disemba kwa kujipatia aslimia 45 ya kura. Juhudi za kidiplomasia za kumshawishiA� Jammeh kukubali kushindwa kwenye uchaguzi huoA� hazijafanikiwa. Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya mataifa ya magharibi-ECOWAS ambayo ilianzisha harakati hizo , imetishia kutumia vikwazo kumshinikiza Jammeh kuondoka mamlakani.