Mkuu wa Sheria Githu Mwigai Kuthibitisha Msimamo wa Kenya Kuhusu Uhusiano kati yake na ICC

Mkuu wa sheria Githu Muigai leo anatarajiwa kuthibitisha msimamo wa Kenya kuhusu uhusianoA� kati yake na mahakama ya ICC.A� Hayo yamejiri kufuatia kutamatishwa kwa kesi dhidi ya naibu Rais William Ruto mapema mwezi huu na tangazo la Rais Uhuru Kenyatta kwamba hakuna Mkenya mwingine ambaye atapelekwa katika mahakama ya ICC.

Muigai amesema wakenya watatu ambao mahakama ya ICC inataka ikabidhiwe kwa madai ya kuwavuruga mashahidi watafunguliwa mashtaka humu nchini na kwambaA� Bensouda anapasa kuwasilisha ushahidi alionao.

Wiki mbili zilizopita mkuu wa sheria alitangaza kwamba serikali hivi karibuni itabuni kitengo cha kesi za uhalifu wa kimataifa ili kushughulikia kesi kuhusu uhalifu unaohusiana na uchaguzi.

Kesi za Kenya katika mahakama ya ICC zilihusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mawaka wa 2007 na kukosa kwa Kenya kubuni jopo maalum la humu nchini kushughulikia kesi kuhusiana na ghasia hizo jinsi ilivyopendekezwa na tume ya Waki.