Mkutano wa madhehebu mbali mbali wa wanawake wavurugwa Kisumu

Mkutano wa madhehebu mbali mbali wa wanawake ulioandaliwa huko Kisumu kukadiria ghasia za kijinsia zilizoshuhudiwa wakati wa ghasia za kisiasa hivi majuzi ulikumbwa na mtafaruku baada ya habari kuenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba hafla hiyo ilikuwa ya ununuzi wa vitambulisho. Kundi la vijana lilivamia hoteli ya Jumia, ambako mkutano huo uliandaliwa, na kuutibua. Vijana hao waliozusha fujo kisha walienda kwenye ukumbi wa kutoa mafunzo, kuwahangaisha wanawake na kurusha viti kabla ya kuwaibia rununu na vipakatalishi vyao. Polisi waliagizwa kufika mahala hapo kuwaokoa wanawake hao na walilazimika kurusha vitoa machozi na kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya vijana hao. Wawili kati ya washiriki kwenye mkutano huo walipelekwa hospitalini kwa matibabu. Jacklin Atieno, ambaye alikuwa akihudhuria mkutano huo, alisema mkutano huo haukuhusu ununuzi wa vitambulisho. Mwishoni mwa wiki Johnstone Muthama wa muungano wa NASA alidai kwamba serikali kwenyeA�A�njama yake ya kubakia mamlakani, inanunua vitambulisho na akawahimiza wafuasi wao kuwa macho na kukabiliana na njama kama hizo.