Mkutano uliosubiriwa kati ya IEBC na vyama vya Jubilee na NASA haukufanyia

Mkutano uliokuwa umesubiriwa kwa hamu kati ya tume ya uchaguzi ya IEBC na chama cha JubileeA� pamoja na muungano wa Nasa kujaribu kutatua mzozo kuhusu matayarisho ya uchaguzi mpya wa urais,haukufanyika baada ya Jubilee na Nasa kudai kwamba hawakuarifiwa mapema. Kulingana na vyama hivyo, stakabadhi ya kurasa kumi iliyotolewa kwao na tume ya IEBC inahitaji muda kutathminiwa. Awali vinara wa Nasa wakiongozwa na Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Musalia MudavadiA� waliondoka kwenye mkutano huo baada ya waakilishi wa Jubilee kukosa kufika. Musalia alilalamika kwamba chama cha Jubilee hakikuzingatia mwaliko huo wa IEBC. Naibu rais William Ruto na kundi lake hatahivyo aliwasili muda mfupi baada ya viongoziA� hao wa Nasa kuondoka kutoka afisi za IEBC. Naibu rais alisema walichelewa kwa kuwa walikuwa wakihudhuria mkutano wa wabunge wa Jubilee katika ikulu ya Nairobi ambao ulichukua muda mrefu. Ruto alihimiza tume ya IEBC kupanga mkutano mwengine wa pamoja katika harakati za kutatua maswala nyeti kuhusiana na uchaguzi ujao wa urais wa tarehe 17 mwezi ujao. Mkutano huo unaotarajiwa kuandaliwa baadaye juma hili .