Mkutano baina ya IEBC, Jubilee na NASA kuahirishwa na kuandaliwa leo asubuhi

Mkutano baina ya tume ya IEBC na Jubilee na muungano wa NASA uliahirishwa jana ambapo utaandaliwa leo asubuhi. Mkutano huo uliahirishwa baada ya muungano wa NASA kuibua wasiwasi kuhusu mswada ulio bungeni unaotafuta kurekebisha sheria ya uchaguzi. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ,anahitaji kudurusu mswada huo ambao utakuwa sehemu ya mjadala wao. Katika mkutano wa jana, muungano wa NASA uliwakilishwa na mkurugenzi wake mkuu Norman Magaya, seneta James Orengo na wakili Paul Mwangi. Nacho chama cha Jubilee kiliwakilishwa na katibu wake mkuu Raphael Tuju, seneta Kipchumba Murkomen na ajenti mkuu wa rais Davis Chirchir.