Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Ya Kenya Power, Dkt, Ben Chumo

kenya-power

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Kenya Power, Dkt. Ben Chumo, amewaambia wanakandarasi wanaotekeleza awamu ya kwanza ya ule mradi wa usambazaji umeme wa Last Mile Connectivity kukamilisha kazi yao ya kuunganisha umeme kwa makazi elfuA�mia tatu na kumi na nne,A�kufikia mwisho wa mwezi Aprili mwaka ujao.

Akiongea wakati wa mkutano wa kutathmini utenda kazi katika mradi huo ulioandaliwa katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Nairobi, Dkt. Chumo, alisema wenye kandarasi wa mradi wa last Mile Connectivity ambao watakamilisha kazi yao kwa wakati watapewa fursa ya kwanza kwenye awamu ya pili ya mradi huo wa shilingi bilioni 63.5.
Alisema mradi wa serikali uliosubiriwa kwa hamu wa Last Mile umeanza kushika kasi huku wenye kandarasi wakisambazaA�A�nyaya za umeme kutoka mitambo 5,320 ya transfoma katika sehemu tofauti za nchi.
Mradi wa last Mile Connectivity unaambatana na mpango wa serikali wa kuimarisha usambazaji umeme hapa nchini hadi kiwango cha asimilia 70 kufikia mwaka ujao ili kuafikia lengo la kuwasambazia wote umeme kufikia mwaka wa 2020.