Mke wa rais wa zamani wa Marekani Barabara Bush afariki dunia

Aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Marekani na mtetezi wa maswala ya elimu Barabara Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.Barabara Bush alikuwa mkewe George HW Bush,babayeA� GeorgeA� Bush. Bi.Bush ,ambaye alikuwa mama wa taifa kati ya miaka ya 1989 hadi 1993 amekuwa akiugua kwa muda na hata kukataa matibabu kabla ya kifo chake.

Salamu za rambi rambi zimemiminika kutoka pembeA� nyingi za ulimwengu kumwomboleza Barabara Bush.A� Mwanawe George HW Bush, George Bush alichaguliwa kuwa rais mnamo mwaka wa 2000 na kuhudumu kwa vipindi viwili kama rais wa 43 wa Amerika.

Marehemu Barabara Bush alijishughulisha na mambo mengi licha ya kuwa mke wa rais ,ambapo alibuni wakfu wa Barabara Bush kusaidia kuinua viwango vya elimu miongoni mwa wazazi na watoto waliotelekezwa katika jamii.Kwenye taarifa kutoka Ikulu ya White House Rais Donald Trump alisema marehemu Barabara Bush atakumbukwa kutokana na uzalendo wake kwa taifa la Marekani na kujitolea kwake kuihudumia jamaa yake.