Mjadala wa wagombea urais unafanyika leo usiku

Mjadala wa wagombea urais umepangiwaA�kufanyika leo usiku katika chuo kikuu cha Kikatoliki cha Afrika mashariki, eneo la Karen, kaunti ya Nairobi. Awamu ya kwanza ya mjadala huoA�inatarajiwa kuanza mwendo wa saa kumi na moja na nusu jioni na itawashirikisha Ekuru Aukot wa chama cha Thirdway Alliance, Abduba Dida wa Alliance for Real Change na Cyrus Jirongo wa chama cha United Democratic. Wengine ni wagombea huru wakiwemo Joseph Nyagah, Michael Wainaina na Japheth Kaluyu. Na awamu ya pili inatarajiwa kuanza saa mbili usiku na itahusisha rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake wa muungano wa NASA Raila Odinga. Awali Rais Kenyatta alisema hatashiriki katika mjadala huo na haijulikani iikiwa amebadili mawazo yake. Hata hivyo Raila amesema yuko tayari kushiriki katika mjadala huo kumkabili rais Kenyatta kuhusu maswala mbali mbali. Mjadala huo uligawanywa katika awamu mbili kuambatana na matokeo ya kura ya maoni yaliyoonyesha kwamba wagombeaji wengine sita hawajapata zaidi ya asilimia tano.