Mizozo Katika ODM Inasababishwa Na Ukosefu Wa Demokrasia, Asema Gideon Mung’aro

Aliyekuwa kiranja mkuu wa wachache katika bunge la taifa Gideon Mung’aro amesema mizozo inayokumba chama cha ODM kwa sasa inasababishwa na ukosefu wa demokrasia katika chama hicho. Munga��aro amedai kuwa amehangaishwa na kiongozi wa chama hicho kila anapotafuta fursa ya maendeleo kutoka kwa serikali. Amewahimiza wakazi wa Kilifi kuunga mkono serikali kwa ajili ya maendeleo.

Haya yamejiri huku baadhi ya wabunge wa muungano wa CORD kutoka eneo la Magharibi wakiongozwa na Seneta wa Kaunti ya Kakamega Bonny Khalwale wakisema baadhi ya viongozi wa CORD wameshawishiwa na muungano tawala wa Jubilee. Mbunge wa Funyula Dr. Paul Otuoma tayari amejiuzulu kama Naibu Mwenyekiti wa chama cha ODM huku mwenzake wa Budalanga��i Ababu Namwamba akitafakari kutafuta chama kipya baada ya kujiuzulu kama Katibu Mkuu wa chama cha ODM. Dr. Khalwale amesema muungano wa Jubilee umejitolea kufanya kila uwezalo kuhakikisha unashinda uchaguzi mkuu ujao.