Misa ya wafu yafanyika shule ya wasichana ya Moi

Misa ya wafu kwa wasichana tisa walioaga dunia katika shule ya upili ya wasichana ya Moi jijini Nairobi imeandaliwa leo shuleni humo. Misa hiyo inahudhuriwa na wanachama wa bodi ya usimamizi wa shule hiyo, wanafunzi na marafiki wa shule hiyo. Miili ya wasichana hao tisa ilitambuliwa jumanne wiki hii baada ya uchunguzi wa DNA kukamilika. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza anayedaiwa kuwasha moto huoA� anakabiliwa na mashtaka-9 ya mauaji. Msichana huyo aliye na umri wa miaka-14 alifikishwa mbele ya jaji Luka Kimaru hapo jana ambako alikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki-2. Kesi hiyo itatajwaA� siku ya ijumaa. Msichana huyo anawakilishwa na wakili Stanley Kangahi aliyeihakikishia mahakama kwamba atahakikisha msichana huyo anafika mahakamni pindi anapohitajika hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa. Vyombo vya habari havikuruhusiwa kuhudhuria kikao cha kesi hiyo ili kulinda haki za msichana huyo ambaye ni mtoto.