Miili Ya Waathiriwa Wa Ajali Ya Naivasha Yatambuliwa

Miili thelathini ya waathiriwa wa ule mkasa wa moto uliotokea kwenye ajali ya Karai huko Naivasha imetambuliwa kupitia uchunguzi wa DNA. Hata hivyo miili tisa zaidi ya watu walioteketea vibaya itachukua muda kuitambua. Mkurugenzi wa kituo cha kitaifa cha kukabiliana na mikasa Nathan Kigotho alisema kuanzia kesho famiia za waathiriwa zinaweza kuchukudnaa miili ya wapendwa wao ili kwenda kuizika. Alisema serikali itagharamia malipo ya kuhifadhi maiti na ya uchunguzi wa DNA na kila familia iliyoathiriwa itapewa shilingi elfu hamsini za kugharamia mazishi.Watu arubaini na tatu waliaga dunia kwenye ajali hiyo iliyotokea tarehe 11 mwezi huu wakati lori moja lililokuwa likisafirisha bidhaa zinazoshika moto haraka lilipohusika kwenye ajali na moto kulipuka na kuyateketeza magari mengine kumi na tatu.