Miguna Miguna akamatwa kwa kushiriki katika uapisho usio halali

Miguna Miguna aliyejitangaza kuwa mfuasi sugu wa kundi la NRM amekamatwa. Miguna alikamatwa leo asubuhi muda mfupi baada ya kudokeza kuwa polisi walivamia nyumba yake. Mkurugenzi wa idara ya upelelezi, NRM alithibitisha kuwa Miguna alikamatwa kwa sababu ya kushiriki katika uapisho usio-halali na kuwa mwanachama wa kundi la NRM lililoharamishwa. Mwanachama huyo wa upinzani ambaye pia alikuwa mwaniaji wa ugavana wa Nairobi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 alichukuliwa nyumbani kwake katika mtaa wa Runda na maafisaA� kutoka vitengo maalumu vya idara ya upelelezi. Hapo jana,A�Miguna aliwashtumu polisi kwa kumkamata mbunge wa Ruaraka, TJ Kajwang kuhusiana na uapisho waA�Raila Odinga. Duru zimearifu kwamba Miguna atashtakiwa kwa makosa sawia na yale yanayomkumba Kajwang, kwa kuidhinisha kuapishwa kwa kiongozi wa NASA na hivyo kusabababisha atekeleze kosa la uhaini. Wakati wa hafla hiyo ya uapisho mnamo Jumanne, A�Miguna ndiye aliyetia saini cheti kilichokabidhiwaA�Odinga kuwa rais wa wananchi.