Mgomo wa wauguzi waingia siku ya nane

Mgomo wa wauguzi umeingia siku yake ya nane leo huku huduma za afya A�zikikatizwa katika hospitali nyingi hapa nchini. Huku mgomo huo ukiendelea kuathiri taifa hili, muungano wa vyama vya wafanyikazi-COTU umejitolea kuongoza juhudi za upatanishi baina ya wauguzi na mwajiri wao. Benson Okwaro ambaye ni afisa wa COTU alisema mashauriano hayo, yataandaliwa jijini Nairobi siku ya Jumanne ambapo maafisa kutoka wizara ya leba na wale wa chama cha A�wauguzi nchini wanatarajiwa kushiriki. Mgomo huo umeathiri utoaji huduma za afya katika hospitali za umma hapa nchini, huku wauguzi wakitaka mwajiri wao atie sahihi na kuidhinisha mkataba wa pamoja ulioafikiwa mwaka uliopita katika mahakama ya maswala ya wafanyikazi. A�