Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu kuendelea

Wahadhiri wa vyuo vikuu kote nchini wameapa kuendelea na mgomo huku wakipuuzilia mbali madai kuwa chama cha wahadhiri (UASU) kimegawanyika. Katibu mkuu wa chama hicho Constatine Wesonga amesema hakuna mgawanyiko katika chama hicho, na kwamba kitaendelea kushinikizwa kutekelezwa kwa matakwa yao. Akiongea na wanahabari,A� Wesonga alisema wahadhiri hawajapokea mawasilianoA� rasmiA� kutoka kwa wizaraA� ya elimu kuhusu kutolewa kwa shilingi bilioni 5.2 na wizara ya fedha ndipo kisitishe mgomo huo ,ambao umetatiza masomo katika vyuo vikuu kwa muda wa mwezi mmoja sasa. Kadhalika aliwahimiza wahadhiri kutorejea kazini hadi serikali itakapotekeleza mkataba wa makubaliano ya pmaojaA� wa mwaka 2013/2017.Malalamishi ya Wesonga yanajiri huku kukiwa na taarifa wizara ya fedha imeidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 5.2 kwenye barua iliyoandikwa tarehe 6 mwezi huu, ambazo ni sehemu yaA� shilingi bilioni 10 zilizoafikiwaA� kwenye mkataba huo.