Mgomo wa wahadhiri umeingia siku ya sita

Mgomo wa wahadhiri umeingia siku yake ya sitaA� huku wahadhiri hao wakikariri kwamba hawatarejea kazini hadi makubaliano yao ya pamoja kuhusu mishahara ya mwaka 2013/2017 yatakapotekelezwa.Katibu mkuu wa tawi la chama cha cha Uasu katika chuo kikuu cha Pwani Chris Ngeng alisema hawatarejea kazini hadi matakwa yao yatakapotimizwa.Wahadhiri wa chuo kikuu cha Pwani walijiunga na wenzao kote nchini huku wanafunzi wakitoa wito kwa serikali kushughulikia malalamishi ya wahadhiri ili waweze kuendelea na masomo yao. Mambo yalikuwa hivyo hivyo katika chuo kikuu cha Masinde Muliro ambapo shughuli za masomo zilikatizwa kufuatia mgomo huo wa wahadhiri. Akiwatubia wanahabari,katibu mkuu wa tawi la Uasu la chuo hicho Prof. Sammy Kubasu alisema kwamba mgomo huo ulioanza tarehe moja mwezi huu,utaendelea hadi serikali itakapotekeleza kikamilifu makubaliano hayo ya pamoja yaliotiwa sainiA� mwezi march mwaka huu.