Mgomo Wa Madaktari Wasababisha Wagojwa Kutoroka Mathari

Zaidi ya A�wagonjwa 100 wenye akili taahira katika hospitali ya Mathari jijini Nairobi wametoroka kutoka hospitali hiyo kufuatia mgomo wa madaktari na wauguzi ulioanza hivi leo. Kufuatia kutoroka kwa wagonjwa hao polisi wameanzisha oparesheni makhsusi ya kuwakamata na kuwarejesha wagonjwa hao hospitalini ili waendelee kutumia dawa zao. Madaktari na wauguzi walianza mgomo wa kitaifa baada ya mashauri yalioitishwa na wizara ya afya kusambaratika jana jioni. Kwenye mkutano na wanahabari jana usiku, waziri wa afya Cleopa Mailu A�alisema wizara hiyo ilitarajiwa kukutana na maafisa wa chama cha madaktari saa kumi na moja jioni lakini maafisa hao hawakuhudhuria mashauri hayo. Mailu alisema ilani ya mgomo ya chama cha taifa cha wauguzi na kile cha madakatari na wauzaji dawa ilitolewa mapema kwani siku 90 ambazo mahakama iliwapa maafisa wa afya na serikali kushauriana na kuafikia makubaliano ya pamoja hazijakamilika.Wizara ya afya, wizara ya fedha, baraza la magavana na tume ya kuratibu mishahara zilikuwa na mkutano wa siku kutwa jana kuhusu mgomo huo uliotarajiwa. Kwenye mkutano huo, mwenyekiti wa tume ya kuratibu mishahara, Sarah Serem, aliwasilisha hati inayoratibu mishahara ya maafisa wa afya, ambayo wizara ya fedha ilisema inaweza kutekelezwa lakini kwa awamu.