Mgomo Wa Madaktari Ungali Unaendelea

Magavana kote nchini wamehimizwa kutafuta suluhu kwa mgomo unaoendelea wa madaktari ambao umelemaza huduma za matibabu na kusababisha masononeko kwa wagonjwa. Viongozi wa kaunti ya Kiambu wakiongozwa na mbunge wa Limuru Mhandisi John Kiragu Chege, wanasema magavana wana wajibu mkubwa wa kutekeleza ili kukomesha mgomo huo. Akiongea katika vituo kadhaa vya kibiashara katika eneo la Limuru wakati alipowakabidhi hundi watu wasiojiweza katika jamii, Kiragu aliubeza mrengo wa CORD kwa kuitisha migomo ya mara kwa mara wakati taifa hili linapokumbwa na mizozo. Kiragu alisema ipo haja ya kuweka mfumo wa jadi kutumika sambamba na ule wa kidijitali wakati wa uchaguzi mkuu, ili kuhakikisha shughuli hiyo inaendelea ipasavyo.