Mgombezi Wa Urais Donald Trump Akashifiwa Na Wenzake

Wawaniaji tikiti ya urais wa chama cha Republican, Ted Cruz na Marco Rubio wamemkashifu vikali mpinzani wao Donald Trump. Wawaniaji hao wawili wanalenga kupunguza umaarufu wa Trump anayepigiwa upatu wa kunyakua tikiti ya chama cha Republican. Maswala ya uhamiaji, afya na ushawishi wa raia wa asili ya Kitaliano yaliangaziwa pakubwa kwenye mjadala kati yao. Kwa zaidi ya saa mbili, Marco Rubio na Ted Cruz walimhoji vikali Trump. Walikashifu vikali rekodi yake ya kibiashara huku wakihoji sera zake. Licha ya shtuma hizo Trump bado anatarajiwa kuibuka mshindi kwenye kura hiyo ya mchujo ya chama cha Republican kwa vile tayari ana wajumbe 82, Ted Cruz ana wajumbe 17 huku Marco Rubio akiwa na wajumbe-16.