Hillary Clinton,mgombeaji wa urais nchini Amerika,kurejelea kampeini zake

Mgombeaji wa urais nchini Amerika kwa tikiti ya chama cha Democratic,Hillary Clinton amesema atarejelea kampeini zake katika mudawa siku chache zijazo baada ya kupata nafuu,siku chache baada ya kusitishwa kwa kampeini hizo kufuatia agizo la daktari wake.Maafisa wa chama hicho wamesema kwamba mumewe Bill Clinton, ataendelea kumpigia debe huku akiendelea kupata nafuu.

Polisi nchini Zimbabwe wanapanga kupiga maarufuku maandamano katika mji mkuu wa taifa hilo Harare kwa mwezi mmoja kwa mujibuwa arifa moja ya umma iliyotolewa leo na kamanda wa polisi nchini humo Newbert Saunyama. Hata hivyo mawakili wa upinzani wamesema kuwa hatua hiyo haifai na inarejesha nyuma hatua zilizopigwa katika kuimarisha idara ya polisi nchini humo.