Mgombea wa chama cha Republican apigwa mweleka katika uchaguzi Alabama

Rais Donald Trump wa Marekani amejitenga na Roy Moore, ambaye alikuwa mgombea useneta wa jimbo la Alabana wa chama chake cha Republican ambaye alishindwa kwenye uchaguzi huo wa kihistoria. Ushindi wa Doug Jones wa chama cha Democratic unapunguza wingi wa wajumbe wa bunge la seneti wa chama hicho kwa wajumbe 51 kwa 49. Jambo hilo linaonelewa na wadadisi wa maswala ya kisiasa kuwa huenda likatatiza mpango wa Trump wa kutaka kufanya marekebisho ya kisheria. Kampeini ya Moore ilikumbwa na madai ya ubakaji yaliotolewa na wanawake kadhaa, japo aliyakanusha.Jones ni mgombea wa kwanza wa chama cha Democratic kushinda kiti cha useneta katika jimbo la Alabama katika muda wa miaka 25.Licha ya wanasiasa maarufu kumtelekeza Moore wakatyi wa kampeini baada ya madai hayo kutolewa hadharani,Rais Trump alimuunga mkono na hata kurekodi ujumbe wa kumpigia debe uchaguzi wa jimbo hilo ulipokuwa unakaribia. Hata hivyo kwenye ujumbe wake wa kwanza kwenye mtanndao wa Twiter, Trump alimpongeza Jones,mgombea kiti hicho wa chama cha Democratic. Aliwakumbusha wafwasi wake kwamba awali alimuunga mkono Luther Strange, mpinzani wa More wa chama chake cha Republican kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama hicho.