Mfungwa Aliyakaa Gerezani Muda Mrefu Zaidi Anyongwa

Jimbo la Georgia nchini Marekani limemuuaa mfungwa wake wa hukumu ya kifo ambaye amekuwa gerezani kwa muda mrefu zaidi. Brandon Astor Jones wa umri wa miaka-72 alihukumiwa kifo miaka-36 iliypoita kwa mauaji ya meneja wa duka wakati wa kisa cha wizi wa mabavu. Adhabu hiyo ilicheleweshwa kwa saa kadhaa baada ya mawakili wake kuwasilisha rufaa dakika za mwisho mwisho katika mahakama ya juu. Astor aliuuwa kwa kudungwa shindano ya sumu mapema leo katika gereza la Jackson. Yeye na mwanamume mwingine Van Roosevelt Solomon walihukumiwa kifo kwa mauaji ya meneja wa duka, Roger Tackett mwaka wa 1979. Solomon aliuawa mwaka wa 1985. Jaji mmoja wa mahakama kuu katika jimbo hilo alikuwa amebatilisha hudumu dhidi ya Astor mwaka wa 1989 akisema kwamba waamuzi wa kesi dhidi yake waliingiza mahakamani bibilia ambayo huenda ilishawishi uamuzi wao.